rightclick logo
::www.rightclicktz.com

Historia ya kompyuta

kizazi cha kwanza <<

>Kizazi cha Pili

Mwaka 1959, Maabara ya MIT ya Servomechanisms walionyesha kwa vitendo jinsi kompyuta inavyoweza kusaidia katika uzalishaji viwandani. Walitengeneza vifaa vilivyokuwa vinaongozwa na kompyuta iliyokuwa ikitumika kuongozea mashine ya kusaga iliokua imeprogramiwa na lugha ya APT.
Kompyuta kubwa za IBM 7000 zilikuwa kompyuta kubwa(mainframes)za kwanza kutengenezwa na IBM zikitumia Transista. Mashine zote zilikuwa zinafanya kazi kwa ufanisi zaidi kuliko zile zilizotumia vacuum tubes. Mbali na hizo IBM 7000 kulikuwa na moja iliyoitwa IBM 7030 ambayo pia ilijulikana kama ‘Strecht’. Hizi zilitengenezwa tisa na kuuzwa kwenye maabara za taifa na kwa watumiaji wengine wa kisayansi walizinunua. Na huu ndo mwaka ambapo ERMA, njia ya kopmyuta ya kurekodi mambo ya kimahesabu, ilianza kutumika kukagua cheki za benki katika Benki ya Marekani kwa kutengeneza maandishi yaliyokuwa yanaweza kusomeka na kompyuta. Kifaa maalumu cha kusomea (Scanner) kilitumika kusoma namba zilizoandikwa katika cheki.

Mwaka 1960, kompyuta ndogo (mini compyuta) aina ya DEC PDP-1 iliuzwa kwa $120000. Moja ya kompyuta kati ya 50 zilizotengenezwa, ilikuwa na ‘cathode ray tube’ moja kwa ajili ya ‘monitor’, ilikuwa haihitaji kiyoyozi na ilikuwa inaweza kuendeshwa na mtu mmoja tu. Uwezo wake mkubwa ulichochea waandika programu wa kwanza kutengeneza ‘video game’ iliyojulikana kama ‘SpaceWar’. Hii ilitumika kwenye kompyuta zote 50 zilizotengenezwa. Na huu ndo Mwaka ambapo Timu iliyoundwa na wanasayansi kutoka kampuni mbali mbali za kompyuta na makao makuu ya jeshi la Marekani Pentagon walitengeneza lugha ya kuprogramu aina ya COBOL ambayo kirefu chake ni Common Business Oriented Language. Ilitengenezwa kwa matumizi ya kibiashara, ilikuwa na lengo la kurahisisha matumizi ya kompyuta. Watengenezaji walikuwa na lengo la kuifanya COBOL ifanye kazi kwenye kompyuta yoyote ile ili mradi tu iwe na ‘compiler’ yake. Mmoja wa watengenezaji aliyeitwa Howard Bromberg alihofia kuwa COBOL huenda isifike mbali, lakini mpaka leo COBOL ipo.
LISP ndiyo iliyokuwa lugha ya kwanza ya programu kutumika kutengeneza programu zilizohusiana na roboti. Ikiwa imetengenezwa na John McCarthy, LISP iliwapa urahisi wanaondika programu.


Kulingana na jarida lililojulikana kama Datamation, IMB ilikuwa na hisa 81.2% katika soko la kompyuta hapo mwaka 1961, mwaka ambao ilitoa kompyuta zake za IBM 1400. Kompyuta moja wapo, IBM 1401, ilitumia transista ndogo na zinazoaminika zaidi na ilitumia kumbukumbu iliyotumia teknolojia ya ‘magnetic core’ (magnetic core memory).
Mahitaji ya soko yalifanya kompyuta zaidi ya 12000 kutengenezwa na hivyo kukawa na haja ya kutengeneza kompyuta kwa ajili ya matumizi mbali mbali badala ya kompyuta zilizokuwa zinatumika kwa ajili ya kazi moja tu.
Mwaka 1962, Timu iliyoongozwa na Tom Kilburn walitengeneza ‘virtual memory’ katika chuo cha Manchester. ‘Virtual Memory’ iliruhusu kompyuta kutumia sehemu ya kuhifadhi data kama sehemu ya kumbukumbu na kufanya kompyuta kufanya kazi kwa haraka zaidi. Na Mwaka huo, Maabara ya LINC (Laboratory Instrument Computer) walitengeneza mashine ya maabara iliyokuwa na uwezo wa kutoa majibu hapo hapo baada ya kupokea vipimo. Ikiwa imefikiriwa na Wesley Clark wa maabara ya Lincoln, ilifanywa kuwa ya biashara baadaye na kuitwa LINC-8.
Mwaka 1963, ASCII – American Standard Code for Information Interchange, iliruhusu kompyuta mbali mbali kutoka kwa watengenezaji mbali mbali kuwabadilishana data. ASCII inahusisha namba 128 zenye muunganiko wa moja na sifuri. Kila muunganiko uliwakilisha herufi katika herufi za kiingereza, alama za kiarabu, na alama nyingine kama za kuuliza n.k.
Na Mwaka huo huo, Watafiti walitengeneza mkono ulioitwa Rancho katika hospitali ya Rancho Los Amigo ya Downey, California kama chombo kwa ajili ya walemavu. Mkono huo wa Rancho ulikuwa na viunganiko sita (six joints) ulikuwa na uwezo wa kufanya kazi kama mkono wa binadamu. Mkono huu ulichukuliwa na Chuo cha Stanford mwaka 1963, ulikuwa kati ya mkono wa kwanza wa ki-roboti uliokuwa ukiongozwa na kompyuta.
Mwaka 1964, Thomas Kurtz na John Kemeny walitengeneza BASIC, lugha rahisi ya kuprogramu, kwa ajili ya wanafunzi wao katika chuo cha Dartmouth. Uwezo wa ku-prosesi data kupitia mtandao ulianza baada ya IBM kutengeneza sistimu ya SABRE kwa ajili ya kufanya ‘bookings’ na ‘reservation’ kwa kampuni za ndege.
Ikitumia laini ya simu, SABRE iliunganisha kompyuta zaidi ya 2000 katika majiji 65. kompyuta zote ziliunganishwa katika kompyuta kubwa mbili (main frame) za IBM 7090, na zilikuwa na uwezo wa kusafirisha data kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa muda wa sekunde tatu.


Kompyuta Supa aina ya CDC 6600 ilibuniwa na Seymour Cray, ilikuwa na uwezo wa kufanya mahesabu hadi milioni kwa sekunde, spidi mara tatu zaidi ya kufanya hesabu kulinganisha na mpinzani wake wa karibu zaidi, IBM Stretch. Kompyuta hiyo aina ya CDC 6600 iliendelea kupata heshima ya kuwa kompyuta yenye uwezo zaidi duniani hadi ilipopitwa na mwenzake CDC 7600 mwaka 1968. Sehemu ya uwezo wake mkubwa ulisababishwa na hali ya kuwa na kompyuta ndogo kumi zilizokuwa zinafanya kazi pamoja.
Na huu ndio Mwaka ambapo puku ya kwanza (mouse) ilitengenezwa.

kizazi cha tatu>>



Pekua rightclicktz.com

rightclick footer